Karibu!
Karibu kwenye Mradi wa Bonde la Ufa: tovuti inayokitanisha muingiliano wa jamii, tamaduni na lugha zilizo katika ukanda wa bonde la ufa nchini Tanzania. Eneo la bonde la ufa linaloanzia kaskazini mwa mpaka wa nchi ya Kenya, kupitia mikoa ya Arusha na Manyara mpaka Dodoma, lina idadi kubwa ya watu wa makabila mbalimbali yenye lugha tofauti tofauti. Kiupekee kabisa, eneo hili ni makutano ya lugha toka familia lugha kubwa tatu za lugha barani Afrika – Nailo Sahara, Naija Kongo, lugha zenye asili ya Afrika na Asia pamoja na lugha mbili za “klik” za Hadzape na Sandawe. Lugha hizi mbili ni ‘tengamano’ katika maana kwamba bado haijajulikana kama zinahusiana na lugha yoyote inayozungumzwa.
Mtandao wa utafiti wa bonde la ufa ni kundi la watafiti linalohusika na lugha na tamaduni tofauti tofauti zilizo katika bonde la ufa. Mtando huu wa utafiti ulianzishwa ili kurahisisha ushirikishwaji wa tafiti,kuanzisha ushirika mpya na kutoa fursa ya kuelimishana. Tunawakaribisheni katika tovuti hii, mjifunze mengi kuhusu eneo hili lenye kuvutia ulimwenguni. Jifunze zaidi kuhusu lugha zinazozungumzwa katika eneo hili hapa. Fahamu mengi kuhusu washiriki wa mtandao kupitia hapa. Pitia machapisho yetu ya lugha na tamanduni hapa. Fahamu mipango mbalimbali ya mtandao wa utafiti wa lugha za Bonde la Ufa hapa. Wasiliana nasi kupitia hapa. Hivi karibuni tunaatarajia kuanzisha wavuti blogu. Tafadhari jiunge nasi kupitia kundi la majadiliano la Facebook……..Mradi wa Bonde la Ufa yaani riftolojia |